Lakini kwa bahati nzuri Inonga hakuvunjika, amepata kidonda kilichotokana na msuguano uliojitokeza. Baada ya kukimbizwa hospitali alishonwa nyuzi 13 na usiku uleule aliruhusiwa kutoka hospitali kurudi nyumbani.
Kwa hiyo ataendelea kusafisha kidonda ‘dressing’. Je, atarejea lini uwanjani? Kuna uwezekano mkubwa akaukosa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos lakini baada ya hapo ananasi kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi dhidi ya TZ Prisons [Ligi Kuu] na Al Ahly [African Football League].
- Amhed Ally, Meneja Habari na Mawasiliano Simba.
0 Comments