Sajili walizofanya Yanga katika misimu miwili iliyopita zimewalipa, ni sajili chache sana ambazo zimeshindwa kufikia matarajio ukilinganisha na zile zilizofanikiwa.
Mfano wachezaji waliosajiliwa msimu huu wameonekana kuvutia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Kaizer Chiefs siku ya kilele cha Wiki ya Mwananchi.
Max, Skudu, Yao n.k Yanga hainunui tu mchezaji bali inatengeneza kikosi! Kununua mchezaji ni jambo moja na kutengeneza timu ni jambo jingine. Unaweza kumchukua mchezaji mmoja Yanga ambaye performance yake ni 10/10 huyohuyo ukimpeleka Ihefu atakupa 5/10.
Kwa hiyo kwa misimu hii mitatu Yanga haisajili tu mchezaji bali inasajili mchezaji kwa kuzingatia mahitaji ndani ya kikosi chao.
Inawezekana baadhi ya mashabiki wa Yanga wana hofu baada ya kuondoka Mayele, Feitoto, Bangala n.k hiyo ni kawaida kwenye mpira wa miguu.
Kwa utamaduni ambao Yanga imeutengeneza hata huyu Konkoni ambaye ameingia kwenye kikosi akikutana na utamaduni wa Yanga kwamba kila mchezaji aliyepo Yanga anatakiwa kupambana kwa ajili ya kushinda, basi Yanga itaendelea kufanikiwa.
Itabakia tu kwamba mchezaji mpya anaweza ‘ku-click’ au inaweza kutokea akashindwa ‘ku-click’.
0 Comments