Hot Posts

6/recent/ticker-posts

HII SASA NDIYO TABIA HALISI YA MASHABIKI WA MPIRA WA TANZANIA


Mashabiki wa Tanzania wameshajitengenezea Kichaka chao yaani umeshakuwa ni utamaduni mechi imalizike imefungwa timu yao wakimbilie kwenye mike na kuponda Wachezaji, viongozi hata benchi la ufundi

Wao hawataki kusikia/kuona timu inapoteza hapo kutatafutwa kila aina ya kasoro, watasemwa watu wachawi, hujma imefanyika yaani kila aina ya neno chafu litatafutwa hapo

Hapana, mpira haipo hivyo hakuna mpira wa aina hiyo lazima kufungwa kutokee, sare zipo huwezi kukataa

Moja ya chuki michezoni huanzia huku kwa mashabiki lugha zisizofaa, maneno ya karahaa Shombo n.k

Ukipewa nafasi ya kuzungumza na Mwandishi wa habari lazima ujue unaenda kuongea nini, punguza kuponda, wacha kuongea maneno mabaya haikusadii itakupoteza

Bado safari yetu ni ndefu michezoni kwaiyo tujaribu kurekebishana sisi kwa sisi ili kukiandaa kizazi kijacho kikute hii amani tunalionayo michezoni

 

Post a Comment

0 Comments