Hot Posts

6/recent/ticker-posts

ZUBERI KATWILA KOCHA MSAIDIZI SINGIDA BIG STARS


Wakati klabu ya Ihefu na Kocha Zuberi Katwila wakithibitisha kufikia tamati kwa mkataba baina yao kwa makubaliano binafsi, habari za uhakika ni kuwa kocha huyo anaenda kujiunga na Singida Big Stars kama kocha msaidizi.


Kocha huyo anakaribia kujiunga na Singida ili kusuka benchi jipya la ufundi litakaloongozwa na kocha Ricardo Ferreira huku timu hiyo ikiwa katika mpango wa kuachana na Mathias Lule na Thabo Senong waliokuwa wanaiongoza baada ya kuondoka kwa kocha mkuu Ernst Middendorp.


"Kuna kocha kutoka Brazil anakuja kuchukua nafasi ya kocha mkuu na msaidizi wake atakuwa ni Zuberi Katwila. Mpango wa kumchukua Katwila ulianza muda mrefu, ndio maana tulianza kumchukua kocha wa makipa, Peter Manyika," kimefichua chanzo ndani ya Singida.


Ihefu imeshatangaza kuachana na Katwila aliyekuwa akiinoa kwa miaka mitatu tangu Oktoba 2020 alipojiunga akitokea Mtibwa Sugar, klabu aliyowahi kuichezea enzi zake akisukuma boli uwanjani.


Kocha huyo amesema ."Sijafanya mazungumzo na timu yoyote ila itakayokuwa tayari kunihitaji tukakubaliana mimi niko tayari hata Ihefu naweza kurudi kwa sababu sijaondoka kwa ubaya zaidi ya makubaliano," amesema Katwila, huku Ofisa Habari wa Singida, Hussein Masanza amekiri pamoja na mkakati wao wa kuboresha benchi la ufundi lakini suala la Katwila wanaliona mitandaoni.


"Taarifa za Kocha Katwila tumeziona mtandaoni lakini sisi hatujamtangaza, tupo kwenye mazungumzo ya mwisho na kocha tutakayemleta tena kutoka nje hivyo tusubiri muda utaamua na uongozi tutatangaza," amesema Masanza.
 

Post a Comment

0 Comments