Hot Posts

6/recent/ticker-posts

HAJI MANARA AANDIKA YA MOYONI KUHUSU MUDADHIR YAHYAH WA YANGA NA UFUNDI WAKE KWA SASA


Ni Mchanganyiko wa Sukari na Chumvi, Ni Muunganiko wa Vitunguu Maji na Vitunguu Swaumu, anakupa vitu vyote kwa wakati mmoja, ana seal Movements zote za uwanjani!!

Jicho lako linahitaji utulivu wa sekunde tu kunielewa what I'm talking about !! Ndio maana halisi ya Dynamo Midfielder, ndio tafsiri sahihi ya kiungo wa kisasa.

Fundi hasa na Macontrol Kama yote,lakini hachezi kama Kiungo Mchezashaji pekee, anakuchanganyia na kiungo mzuiaji kwa wakati mmoja.

Dakika moja utamuona kaenda kufanya tackling, Dakika inayofuata kenda kufanya Assist, mara kidogo yupo nyuma kuiokoa team, sekunde inayofuata kaenda kugongesha besela kwenye goli la Mpinzani, Uuhh lalaaa!!

Fo-def ndio kitaaalamu zaidi, anazuia na kushambulia, anafunga na kuokoa, ana assist na kublock, ni Mbaazi kwenye sahani ya Chuma, ni kama ushawahi kumuona Steven Gerrard enzi zake!! Kumuangalia akicheza, ni kama unaila Pilau iliyokolezwa Minyama kwenye Sinia. 

Ooooh My God, kisha jamaa ana ile jeuri ya kizanzibar uwanjani, Eagle ya kiunguja ,Spirit ya Watu wa Visiwani, Soft ukija Soft, Hard ukijitia Mgumu.

Anawazidi Viungo wengi wanaoitwa holding, Coz yeye ana ududu mwingi mguuni, ni key Player wetu sababu offer zake ni nyingi kuliko tunavyodhani.

Haijalishi ni lini lakini Mudathir 'Super' Yahya atajengewa mnara wake nchi hii siku moja, kama sio Dar basi kwao Bububu.

#mudathir_yahya27

 

Post a Comment

0 Comments