Leo naomba tuzungumze kuhusu "Formations and Principles" sababu tumekuwa tukiangalia mechi mbali mbali ila kuna baadhi yao hichi kitu kinawapa shida kuelewa
Mfumo unaweza kubadilika kutoka mechi hadi mechi au wakati mechi inaendelea lakini Kanuni isibadilike! Mfano mzuri nitatoa kwa Antonio Conte, Pep Guardiola, Jose Mourinho na Eric Ten Hag.
Timu inaweza ikaingia uwanjani na mfumo wowote kati ya hii 4-2-3-1, 4-3-3, 4-4-2, 3-4-3 au 3-5-2! Hii mifumo yote inaweza kubadilika kulingana na mazingira ya mechi au mchezo ukiwa unaendelea hapo hapo.
Antonio Conte Kanuni (Principle) yake ni kujilinda zaidi ndani ya uwanja na kuondoka nyuma haraka kwa kasi kwenda mbele(Counter Attacks) ila anaweza kutumia mfumo wowote ule katika kujilinda(4-4-2, 3-4-3 au 5-4-1).
Jose Mourinho naye hana tofauti na Antonio Conte sababu kanuni yake (Principle) ni kujilinda ila mifumo ya kujilinda anaweza akatumia wowote ule kati ya 5-3-2 au 4-3-3.
Hapa tuelewane vyema yani mifumo inaenda inabadilika hivyo anajilinda kwa mfumo wa aina yoyote ile ila kanuni yake inabaki ilivyo na mfumo ndio utaona unabadilika / inapishana.
Pep na Ten Hag wao Kanuni(Principle) yao ni kushambulia zaidi hivyo mfumo wao wa kushambulia unaweza kubadilika kulingana na mazingira ya mchezo husika ila kanuni itabaki ni ile ile.
Pep na Ten Hag wao watashambulia kwa kutumia mfumo wowote kati ya 4-2-3-1, 4-3-3, 3-5-2 au 3-4-3 hivyo Kanuni yao ya kushambulia itasalia ilivyo ijapo Mfumo ndio unaweza kubadilika ndani ya uwanja au mechi hadi mechi.
Hivyo basi kanuni (Principles) haziangalii utatumia mfumo (Formations) gani muhimu ni kutimiza malengo yako ndani ya uwanja kwa kutumia mfumo wowote kwenye kanuni unayoisimamia
Unaweza kuona mfumo upo kiuzuiaji zaidi lakini kanuni ya kocha au timu husika ikawa ni kushambulia na wakayekeleza majukumu yao ipasavyo.
Let's Goo!!.

0 Comments