Hot Posts

6/recent/ticker-posts

STORY YA MWANDISHI WA CLOUDSFM KUHUSU SIMBA INAWEZA IKUTOE MACHOZI


Wakati narecord hii video hapa Lupaso Vijana wa Kitanzania wakifanya mazoezi nilivutiwa na Kijana ambaye alipewa bendera ya Simba katika zile bendera za klabu nane, namna alivyokuwa haiweki chini na anaikumbatia kwa mahaba makubwa sana. 

Its lonely at the top! Yupo peke yake ukanda wa CECAFA, wapo watatu tu Kusini mwa Jangwa! Againts the odds anapambana, against the OGS aliitwa Underdog lakini Script kutoka bonde la Mto Msimbazi inaendelea kuandikwa. 

Nikawatazama kwa haraka Vijana wadogo sana zaidi ya 1,000 ambao ni Watanzania wenzetu wanaingiza siku yao hapa kupitia football na Simba ndio sababu, nikatazama walivyo na nuru na wanaamini watafanikiwa, ni mpira na ni Simba sababu ya haya yote. 

Wakati naitazama bendera ya Simba ambayo ni timu yangu ikipepea nilikuwa najisemea tu moyoni kuwa In shaa Allah nitakuwepo siku hiyo kuishuhudia hii klabu ambayo niliipenda sana kwa moyo wote licha ya familia kuwa Yanga tupu. 

SIMBA kwangu mimi ni kama hawa Vijana ni mfumo wao wa maisha, niliingia Media kutokana na Ushabiki wa hii timu! Mitaa ikaniamini na kunivisha joho la kuwa Mwandishi wa Habari, ni Simba hii inafanya nipate mkate na rizki ya kusukuma familia, siwezi jua ningekuwa wapi leo. 

Kwangu hii timu inanidai mengi sana na huwa najitahidi niwezavyo kukumbuka nilipotoka, sadaka ya pekee kwangu ni kukiri kuwa hii ni timu yangu popote pale, nimewahi kukosa rizki kadhaa kisa kuwa wazi lakini Alhamdulillah nimepata mengi kupitia hii timu. 

MUNGU IBARIKI HII TIMU, KWANGU NI ZAIDI YA KLABU NI MFUMO WANGU WA MAISHA🙏❤️ Siidai chochote ila yenyewe inanidai mengi.

More than a Club! Its my lifestyle! This my team! 


Post a Comment

0 Comments