Hot Posts

6/recent/ticker-posts

GADIEL MICHAEL NA NJIA YAKE SINGIDA


GADIEL MICHAEL — Beki huyu alitua Simba kwa mbwembwe kubwa akitokea Yanga 2019 wakati huo akiwa na uhakika wa kucheza beki wa kushoto kutoka na mahitaji ya kikosi hicho tofauti na sasa.
.
Kutokana na Ubora mkubwa ambao Simba walikuwa nao wakati huo hakuna mchezaji ambaye hakutamani kukipiga Msimbazi kwa kuwa mafanikio yalionekana ndani na hata nje. Gadiel hakuangalia ushindani wa namba uliokuwepo Simba kwa Mohamed Hussen ‘Tshabalala’, akaona ni vyema akatimiza lengo la kwenda kukipiga Msimbazi.
.
Msimu uliopita baada ya kumalizika kwa mkataba wake uongozi wa Simba ulitangaza kumuacha na sasa ndiye nahodha wa Singida Big Stars ambako ni panga pangua anaanza kikosini. Licha unahodha tu, jicho la ARENA express limeangaza katika michezo tofauti ambayo amecheza na kiwango chake kilivyokuwa BORA kwani jamaa anaupiga mwingi na kuwashangaza wengi kutokana na namna ambavyo anasakata kabumbu akiaminiwa na kocha wake. 


 

Post a Comment

0 Comments