Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MWIBA MCHUNGU WA MBARALI ESTATES KWA WANANCHI


Baadhi ya viwanja huwa ni vigumu sana kwa baadhi ya wapinzani. Yaani huwa inakuwa hivyo tu. 

Kwa mfano, Arsenal kwa miaka mingi sana walikuwa hawapati matokeo ya ushindi pale Goodson Park mbele ya Everton mpaka walipofanya hivyo msimu huu. Kwao mechi dhidi ya Everton ugenini imekuwa ngumu licha ya utofauti mkubwa wa ubora kati ya timu hizo.


Mfano mwingine ni jinsi ambavyo Manchester City amekuwa akipata taabu ugenini kwa Wolvermpton Wonderers. Huwa inatokea mara kadhaa timu fulani inakuwa inapata tabu dhidi ya mpinzani fulani mara kwa mara. Na kwa bahati mbaya au nzuri hii huwa inakuwa kama muendelezo fulani. 


Na hii kitu ni mbaya sana kwani huwa inaingia mpaka vichwani mwa wachezaji wakiamini wanaenda kukutana na mpinzani anayewaweza wao tena katika kiwanja ambacho hawana bahati nacho. Na hapa hata hali ya kujiamini ya wachezaji huwa inapungua kuelekea mchezo dhidi ya wapinzani hawa. 


Wakati kwa upande wa pili, wachezaji wa upande mwingine ambao wana historia nzuri na mpinzani huyo hali ya kujiamini kwao huongezeka wakiamini wameshamfunga mara kadhaa hivyo pressure kwao hupungua. Na hapa ndipo siri ilipo.


Ihefu waliamini kama walimfunga Yanga SC msimu uliopita kwenye mazingira kama yale... Kwanini siyo msimu huu?? ...


MBARALI ESTATES.... bado ni mwiba mchungu kwa Wananchi....
 

Post a Comment

0 Comments