Ikiwa tayari hati yake ya kusafiria (Passport) ipo chini ya Al Ittihad Alexandria waliyobaki nayo kimabavu, kumbuka ni timu ya jeshi hii, wanataka Chama asaini mkataba ambao umeandikwa kwa lugha ya kiarabu, lakini alishaupitia na kuona una kasoro nyingi ndani yake, muda umekimbia na hofu imeanza kutanda! Mchezaji bora mwenye maamuzi bora hata kwenye nyakati ngumu.
Baridi imetanda Kaskazini mwa Afrika, nyota Clatous Chama tayari amepishana na Viongozi wa Al Ittihad kwenye mapambano ya rizki, anataka kurejea Zambia haraka iwezekanavyo! Lakini kwanza atoke alipo ili afike Ubalozini jijini Cairo ili apate msaada ndani ya Ubalozi wa Zambia.
Tik tok ticking! Mshale wa saa unakimbia! Anaagiza kwanza chakula ili apate nguvu kabla hajatoka kimagendo ili apate usafiri wa kumtoa alipo, kumbuka hana passport na timu inamtaka awepo kambini na hati yake wanayo, ni saa 3:45 usiku ni Kaskazini mbali na nyumbani kwao Zambia, baridi ni kali na mvua ni kubwa sana.
Nje Police wapo kwenye doria, huku simu za upepo zikiendelea na mawasiliano ya Chama na watu wa Ubalozini na anaowaamini yanaendelea, moja kati ya mission ngumu kuondoka mji mmoja hadi mwingine tena mgeni bila passport, usiku mrefu ambao ni eidha ashinde ama apoteze.
Moja kati ya simulizi nzito ambayo nimeipa jina la THE 17 IMPOSSIBLE kwenye diary ya MAGIC FINGERS! Upo tayari kwa ajili ya hii documentary??____ 😀
0 Comments