Kocha wa Roma, Jose Mourinho amesisitiza bao la Romelu Lukaku sio muhimu baada ya straika huyo kufunga katika dakika ya 82 kwenye ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Empoli. Lukaku alifunga bao lake kwanza akiwa na uzi wa Roma baada ya kujiunga kwa mkopo akitokea Chelsea lakini kocha wake alionyesha kutokuwa na mhemuko.
.
Licha ya kulipuuza bao hilo, Mourinho alimsifu Lukaku kwamba alibadilisha upepo kufuatia ushindi huo mkubwa baada ya kuanza msimu kwa kusuasua. “Bao lake halikuwa muhimu. Inaweza kuwa muhimu kwake, najua mastraika wanaishi kwa sababu ya mabao.” alisema Mourinho.
.
“Tangu alipowasili amekuwa kila kitu kwenye timu, haijalishi kama akifunga au hakufunga. Ni wazi atajisikia furaha baada ya kufunga bao kitu ambacho ni kizuri kwa ajili yake, Lukaku ameleta utofauti kwenye timu na bado tunahiji kujifunza jinsi gani ya kucheza naye, Lukaku anahitaji kufurahi na mashabiki pia wanamkubali,”
0 Comments