Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SHAFFIH DAUDA AANDIKA MAZITO KWA NOVATUS DISMAS




PROJECT THE FUTURE|| Nilikuwa nina ndoto kubwa sana za kuwa Mwanasoka wa kulipwa, ndoto ambayo ilipokea upinzani mkali sana na haikuweza kuchipua ndani yangu, kwakuwa kila nikilala na kuamka bado nilikuwa naliwaza soka la kulipwa, nikasema siku moja nitacheza soka la kulipwa. 

Miaka ikaenda na maisha yakanipa kurasa mpya ambazo nilipaswa kuzisoma kwa sauti ya juu japo maandishi ni ya Kirumi, nikasema wasaa umefika wa Mimi kucheza soka la kulipwa nikiwa na miaka zaidi ya 30, lakini sitoingia uwanjani bali mtazamo wangu, njaa yangu na mawazo yangu yatafanikisha Vijana kucheza soka la kulipwa. 

A dream realised ndani ya @shadakasports na shukrani kubwa kwa Mbwana Samatta kwa kuamini naweza kuwa sehemu ya safari yake, nilimuangalia akitwanga mechi kadhaa ikiwemo ya ubingwa wa Belgium pale Genk, nikamshuhudia Wembley kama Mtanzania wa kwanza kucheza pale, nikamshuhudia siyo tu akiwa Mtanzania wa kwanza kucheza EPL na kupasia nyavu na alinipa nafasi ya kumuona akiwa kama Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya Uefa Champions League, bado ndoto ilikuwa inaishi na kelele zilikuwa zinanijia kichwani kuwa napaswa kuwa Mchezaji wa kulipwa, kila nikilala na kuamka. 

Nikamwona tena mtoto mwingine kutoka mtaani, kisha academy ya Future Stars, Alliance,Azam, Biashara na baadae Israel, Ubelgiji na sasa rasmi Ukraine ndani ya Shakhtar kwa ajili ya Champions League, ndoto inaendelea kuishi ndani yangu, ni kweli sasa nacheza soka la kulipwa kupitia Kurasa mpya nazozisoma. Sasa najiandaa kwenda kuangalia mechi zingine za UCL.

Nikupongeze Kijana wangu @novatus_40 kwa kuiamini @shadakasports na unabaki kuwa kielelezo cha utu, uvumilivu na bidii ya kazi, utasalia kuwa mmoja wa mifano kwa vijana wa kitanzania, The future is now! The future looks Young👊 @2official6

Post a Comment

0 Comments