Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MKUDE NI MTU MUHIMU SANA TAIFA STARS

 



🗣️ Kuelekea katika mchezo wa Taifa Stars dhidi Algeria, Mechi ya kupambania kucheza fainali za Afcon nchini Ivory Coast 🇨🇮, Tayari timu ya Taifa imeshaondoka nchini kuelekea nchini Tunisia 🇹🇳 kuweka kambi kabla ya kwenda Algeria kwenye mchezo husika


🗣️Wadau wengi wameshikwa na ukakasi baada ya kuona jina la kiungo wa Yanga Jonas Mkude kwenye orodha ya wachezaji 25 walioitwa katika kikosi cha Taifa Stars, Mpaka sasa Taifa letu bado limeshindwa kumpata kiungo mwenye tabia kama za Mkude ndio maana ameitwa tena ingawa kwenye klabu yake apati nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza


🗣️Viungo wa kati wako wengi lakini Mkude anasifa pekee ambayo anawashinda viungo wengi, Kama unahitaji timu iwe na uwezo wa kuanzisha mashambulizi kutokea nyuma basi bila shaka lazima umuhitaji mkude kwasababu anauwezo mkubwa wa kushuka chini na kuchukua mipira kwa mabeki na kuisambaza taratibu kwa pasi fupi na kwenda mbele kwa nidhamu kubwa ya kumilika mpira


🗣️Mkude pia kama unajitaji kiungo anaweza kumeza mipira shitukizi ya wapinzani kutokea eneo la kati kabla haijafika kwa mabeki, Mkude anaweza kufanya hiyo kazi kwakua huwa anapenda kuwa mbele ya mabeki na eneo la kati bila kuwa na tamaa ya kusogea mbele zaidi, Pia anauwezo mkubwa wa kuficha mianya ya wazi kati ya mabeki wa kati kwakua anauwezo wa kukaa mbele yao kwa muda mrefu na kumfanya mpinzani ashindwe kupiga pasi za mwisho 



Post a Comment

0 Comments