Hot Posts

6/recent/ticker-posts

LUIS MIQUISSONE NI YULE ILA BOLI BADO SIO LA KIPINDI KILE AJITUME SANA


Nilisema BADO Simba hawajampata Luis Miquissone mwenyewe maana hakuwa tayari ikawa vigumu kueleweka lakini baadaye imedhihirika.


Luis Miquissone ni mchezaji mzuri lakini hakuwa na match fitness ya kutosha kupambana mwanzoni mwa msimu.


Baadaye benchi la ufundi la Simba waneliona hilo na bila shaka wamelifanyia kazi.


Taratibu Simba wataanza kupata ubora wa Luis katika mechi chache zijazo na ninaamini atakuwa na faida kubwa.


Tayari ametumikia timu tatu kubwa zaidi Afrika kutoka katika Kanda za Kaskazini, Mashariki na Kusini kwa maana ya Al Ahly, Simba na Mamelodi.


Maana yake anajua maana ya kuwa mchango na kutegemewa. Naye atakuwa anafanyia kazi kwa juhudi anachopungukiwa na mechi chache zijazo ninaamini tutamuona Miquissone MWENYEWE.


#iamsalehjembe🇹🇿
 

Post a Comment

0 Comments