Hot Posts

6/recent/ticker-posts

PAMBANO LA MWAKINYO LEO NI FULL KIZUNGUMKUTI!


Baada ya jana kuripoti kuhusu kwanini Champez Hassan Mwakinyo hataki kupanda ulingoni leo hii na sababu kuwa ni Promota kutoka kwa chanzo changu, nikapokea taarifa kutoka chanzo cha upande wa pili juu ya kwanini Hassan hataki kupanda, hivyo nakamilisha stori kutoka vyanzo vyote (pande mbili)


- Sababu inadai Hassan ana mgogoro na Mafia Promotions hilo kweli chanzo changu kimekiri na sababu ni kuwa kulikuwa na Watoto kama wawili wa Tanga walikuwa wanatrain kwenye dojo la Hassan akiwemo Salim Mtango ‘Messi wa Boxing’ ambapo wameondoka na kujiunga na Mafia Promotions. 


“Kilichopo ni kuwa Hassan anawabania Ndugu zake wawili kutoka Tanga wasipande ulingoni akiwemo Salim Mtango kutokana na kuwa waliondoka kwake na anawamind Mafia Promotions kutokana na kuwapa thamani kubwa hawa watoto kuliko yeye, hiyo ndio sababu yake kuwabania watoto” kilisema chanzo hicho cha pili. 


Wakati nazidi kuzungumza na chanzo cha pili akaendelea kuniambia “Hassan alishasaini mkataba ambao hauna kona kona na ashalipwa pesa yake yote kwa dola za Kimarekani (anataja) hivyo kilichosalia ni yeye kupigana na sio kuangalia wakina nani watapigana kabla yake kwakuwa sio mkataba wake unavyosema” kilitanabaisha chanzo hicho. 


Katika kuendelea kuhojiana na chanzo hicho cha pili nikamuuliza kuhusu Bondia kubadilishwa hilo lipoje? Akasema namnukuu “Mengine tuyaache tu lakini huyu Bondia wa pili baada ya wa kwanza kuumia (anacheka) tulishirikiana kwenye kumtafuta na tulikubaliana sote wala hapakuwa na kona kona yoyote” kilihitimisha chanzo changu. 


Kwa mujibu wa chanzo cha pili inaonekana Hassan hawezi kupanda ulingoni bila hao Vijana kuondolewa kwakuwa hawapikiki chungu kimoja na Mafia Promotions, hivyo ni kazi kwa Promoter wa pambano kuona namna gani anaokoa jahazi hilo kwakuwa msimamo wa Hassan haubadiliki, amenyooka. 


Hii ni kwa mujibu wa chanzo cha pili ambacho ni kinzani na chanzo cha kwanza! So utata upo hapo. 


VISIT MOROGORO🇹🇿
 

Post a Comment

0 Comments