Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KWA SIMBA HII UENDA IKAPOTEZA KWA POWER DYNAMO

 


🗣️ Huenda klabu ya Simba ikapoteza mchezo wake wa kwanza ugenini dhidi ya Power Dynamos nchini Zambia mechi itakayopigwa tarehe 15 ya mwezi kupambania nafasi ya kwenda hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Africa, Nakumbuka mchezo wa Power Dynamos dhidi ya Simba katika Tamasha la Simba Day na kupata ushindi wa mabao mawili kwa shida katima mchezo huo.

🗣️Kuanzia msimu huu Simba imekuwa ikipata shida kupata matokeo katika mechi zake kuanzania katika mechi za ngao ya jamii kuanzia mechi dhidi ya Singida na mchezo wa fainali dhidi ya Yanga, Pia kwa mechi za ligi kuanzia mchezo dhidi ya Mtibwa sugar na mchezo dhidi ya Dodomajiji klabu ya Simba ilipata matokeo kwa shida sana na kushindwa kuonyesha soka ambalo watu wamezoea kuiona Simba msimu uliopita 

🗣️Kulekea katika mchezo dhidi ya Power Dynamos kocha wa Simba ameomba kupata mechi za kirafiki zisizopungua mbili kwaajili ya kufanya marekebisho yaliyoonekana katika mechi za nyuma, Inasemekana Simba ikacheza katika mechi za kirafiki dhidi ya JKU na KMKM kutokea Zanzibar mechi ambazo huenda zikichezwa katika uwanja unaotumika na klabu ya Simba kwa Mazoezi wa Mo Arena uliopo bunju, Inasemekana kwa kocha mkuu wa Simba Robertinho amegomea mechi hizo kwakua anaona ni mechi zisikuwa zq ushindani na haziwezi kuipa Simba kipimo sahihi kuelekea mchezo dhidi ya Power Dynamos.



Post a Comment

0 Comments