Hot Posts

6/recent/ticker-posts

JE HUU NI MPANGO WA DUNIA KUPOTEZA WACHEZAJI WENYE VIPAJI VIKUBWA VYA SOKA??


Kwasasa Dunia imeamua kuwaweka pembeni wachezaji wenye vipaji binafsi, imeamua kuwapuuza na kuwaondoa kabisa katika Ulimwengu wa soka, Dunia inahusudu zaidi wachezaji wa maelekezo kuliko "Talented".


Alikuwepo Neymar Jr licha ya kuwa na uwezo mkubwa uwanjani bado Dunia haikumthamini, ikamuweka pembeni na sasa ameamua kwenda kula pension zake huko Uarabuni, hivi ni kweli Neymar anaweza kukosa timu ya kucheza Ulaya kwa uwezo wake?


Cristiano Ronaldo ajenda yake ni pana sana na ilichukuliwa kwa upana sana kutokana na ushawishi wake (hili tuliache tu kwasasa), Vinicius Jr pia ni miongoni mwa wahanga wa vipaji vyao, walimbagua, wakatoa kashfa za kila aina lengo ni kumtoa mchezoni na pengine apotee kabisa katika soka lakini imekula nguzo, huwezi jua inawezekana kuna bomu jingine linapikwa kwaajili yake.


Miongoni mwa wachezaji wenye uwezo mkubwa huwezi ukaacha kumtaja Anthony nyota wa timu ya Taifa ya Brazil na Manchester United, wakati anajiunga na United kila mchambuzi alizungumza kuhusu uwezo wake, hawakuangalia kipaji chake bali waliongelea kuhusu kuchelewesha timu [ Hapa maabara imeharibu] bado akawa na msaada wa timu yake ya United na timu ya Taifa ya Brazil.


Njia zote zimeonekana kutokufanya kazi na imeshindikana kumpoteza kwani kila mara amekuwa akiaminiwa na Ten hag, baada ya yote hayo kutokufanya vizuri limekuja hili la unyanyasaji kwa wanawake.


Antony anashtakiwa kwa kosa la kumnyanyasa mpenzi wake wa zamani, tena si shtaka moja ni zaidi ya moja, na shtaka kama hili lilimuondoa Greenwood nyota wa England kwenye ramani ya soka kwa muda mrefu na baada ya kesi yake kusikilizwa akagundulika hana hatia na akapelekwa kwa mkopo Getafe baada ya wafanyakazi wa Man United kugoma asirudi kikosini hapo, huu ni mpango wa Dunia.


Je, huu utakuwa ni mpango wa Dunia kumuondoa Antony kwenye ulimwengu wa soka?
 

Post a Comment

0 Comments