Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MBAPPE APIGWA CHINI NA WACHEZAJI WENZAKE ISHU YA UNAHODHA



Kylian Mbappe amepigwa chini na wachezaji wenzake kwenye mchakato wa upigaji kura kuchagua nahodha mpya wa mabingwa hao wa Ufaransa, Paris Saint-Germain. Kocha wa miamba hiyo, Luis Enrique aliwaambia wachezaji wake anahitaji nahodha mpya wa kikosi chake kwa ajili ya msimu huu na kuwataka wachezaji hao kupiga kura kwa siri kumchagua anayefaa na hapo ndipo jina la Mbappe lilipokatwa, wakilitupa mbali kabisa.

.

Na kwenye mchakato huo, Mbappe aliishia kushika namba nne kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa la RMC Sport. Katika kura za kumsaka nahodha, Marquinhos ametajwa kuwa namba moja, akifuatiwa na Danilo Pereira na namba tatu ni Presnel Kimpembe.
 

Post a Comment

0 Comments