Hot Posts

6/recent/ticker-posts

MANULA NDIYE ALIUWA KIPAJI CHA BENO KAKOLANYA! SOMA HII


 🗣️Toka msimu wa mwaka 2019/2020, Kipa Beno Kakolanya ajiunge na klabu ya Simba akisajiliwa kama mchezaji huru baada ya kuachana na Yanga, Kakolanya alikutana na changamoto kubwa katika klabu ya Simba baada ya kushindwa kumtoa Aishi Manula kwenye lango la Simba na kupelekea kuwa kipa wa akiba au kipa namba mbili kwa muda mrefu katika kikosi hicho cha wanamsimbazi


🗣️ Beno Kakolanya kwa sasa ni kipa wa timu ya Singida big stars, Lakini toka ameanza kucheza katika timu hiyo hali yake inaonekana haiko vizuri hasa kwenye uchezaji wake, Kilawangochake kikochini makosa mengi binafsi yanaonekana kwake, Ukianza kuutazama mchezo wa nusu fainali ya ngao ya jamii makosa mengi kwake, Mchezo wa mshindi wa tatu dhidi ya Azam kwenye ngao ya jamii alifanya makosa mengi mpaka ikapelekea kupoteza mchezo dhidi ya Azam fc, hata katika mchezo wa pili wa kombe la shirikisho barani Africa mabao kwa mabao anayofungwa anaonekana hayuko katika kiwango chake


🗣️Kiwango bora cha Aishi Manula ndani ya Simba ndiyo sababu iliyopelekea kushuka kiwango kwa Beno kwakua alikuwa hapati nafasi ya kucheza hivyo imepelekea kukosa ubora katika mechi na kupungua hali ya kujiamini golini, Nafikili itamchukua muda mrefu kurudi katika kiwango chake tulichozoea kumuona nacho



Post a Comment

0 Comments