Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KILICHO MKUTA FEITOTO SASA KIMEMKUTA PRINCE DUBE NGOMA NI NGUMU


Wakati wa sakata la Feisal Salum nilisema hapa kuwa hakuna mkataba ambao hauvunjiki, kila mkataba lazima uwe na kifungu cha TERMINATION lakini FIFA wameweka wazi vigezo vya mkataba kuvunjwa, tukavisema hapa Watu wakaziba masikio! Time itafika unamtaka Mchezaji wa timu fulani unamshawishi tu waambie hauna furaha uvunje mkataba, hii ni hatari kwa mpira. 

Wakati wa lile sakata nikasema FIFA wanaruhusu mkataba kuvunjwa ila pia lazima kusiwe na INFLUENCE OF THIRD PARTY yani timu nyingine ama Mtu mwingine asiwe shinikizo wa mkataba wa Mchezaji kuvunjwa, FIFA wanasema ikigundulika Mchezaji na timu wanaweza kufungiwa na faini juu, WATU MKAZIBA MASIKIO. 

Nikasema hii itakuja TREND hapa nchini, sio rahisi Mchezaji kusema tu anataka kuondoka na asepe! Imekuja kutokea kwa PRINCE DUBE nae anataka kuondoka Azam FC, hana furaha maybe maana yake ni kuwa Azam wanapaswa kuisaka escape route ya Dube! Wengine wanasema kuna RELEASE CLAUSE unaweza kuiweka kubwa lakini itafika wakati Mchezaji atakuwa hana cha kupoteza, amebaki unamlipa Mshahara na anakujazia nafasi, utashusha bei na ataondoka kwa dau dogo tu. 

Ndio maana wakati ule tulisimama sana na YANGA tukaonekana MIYEYUSHO, leo imetokea kwa Azam kesho itatokea kwa Simba ama Mtibwa! Katikati ya msimu mtu anaomba kuondoka na dirisha lishafungwa hujui cha kufanya! Tuliposimama tuliutetea mchezo pendwa wa mpira wa miguu na sio Mtu wala taasisi. 

ZAKA anasema wanaomtaka DUBE waende, Yanga pia walisema wanamtaka FEI waende! Wametaja na Yanga walitaja dau! Ile script ya mwaka jana kama ya Yanga imejirudia Azam, naomba asicheze Mtu nje ya key! Chukueni upande wa Dube aondoke kama ilivyokuwa awali kwa Feisal, aende huko anapotaka ambapo hatupajui. 

Ule wasaa umefika tena! Same mood, different code! Mchezo unaenda wapi??____

VISIT MOROGORO🇹🇿

 

Post a Comment

0 Comments