Ni vijana wadogo wenye kuijua vyema kazi zao
Afisa habari wa Yanga SC, Ally Kamwe na nduguye Ahmed Ally ambaye yeye ni Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano Simba SC
Wikiendi ijayo timu zao kwa nyakati tofauti zitaingia kwenye pilka pilka tena ya michuano ya kimataifa Klabu Bingwa Afrika hatua ya makundi
Yanga SC wao watakuwa nchini Algeria dhidi ya CR Belouizdad huku Mnyama Simba SC wao watavaana na ASEC Mimosas ya Ivory coast
Napenda namna wanavyoifanya kazi yao kwani kila mmoja amechagua njia yake
Kamwe amechagua kuwa mbunifu zaidi kwa kuleta matukio mbalimbali na imeingia kweli mjini huku Ahmed Ally yeye na KISPIKA cha Mtaa
Yale magoli 5 yanakaa pembeni sasa ni kupambania klabu kwenye engo nyingine, huku kunatafutwa heshima na pesa zaidi
Nitaendelea kuwaombea afya njema na Uhai zaidi kwani kufanya vizuri zaidi hapo mlipo kunatufungulia njia na kuaminiwa sisi vijana kwamba tukiaminiwa basi inawezekana
0 Comments