Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SHAFFIH DAUDA ATOA DARASA ILI UWE MCHEZAJI BORA WA MPIRA HII NDIYO INAHITAJIKA

 

Uploading: 209624 of 209624 bytes uploaded.

Sehemu kubwa ya wachezaji tunaowaona huko duniani ,wamezaliwa na vipaji lakini hawakutosheka na vipaji pekee , unaweza kuwa mchezaji lakini usifikie daraja la kuwa mchezaji bora kama hakuna juhudi binafsi za kujiongezea maarifa , ubora na Ukamilifu wa mchezaji wa mpira unajengwa na vitu vikubwa vinne ! ukiwa mchezaji na una ndoto ya kuwa mchezaji bora hiwezi kuvikwepa ! 


1. Consistent training 

Muendelezo kwenye mazoezi , hauwezi kuwa bora kama utakuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi kwa kujitegea ! Wapo wachezaji wana uwezo wa kuzaliwa nao lakini ukamilifu wa mchezaji kamili ni lazima awe fit , ufit haupatikani nje ya mazoezi ni sawa na kusema practice doesn’t make perfect ,perfect practice dose .unahitaji sana kufanya mazoezi ili kuwa mwenye kiwango bora ! 


2. Mental toughness .

Mchezo wa mpira wa miguu unabebwa sana na utimamu wa akili , kadri unavyoiweka akili mchezoni ndivyo inavyokupa uhakika wa game bora! mara kadhaa utasikia mchezaji fulani hatokuwa sehemu ya mchezo kwa sababu ya matatizo ya kifamilia ,vipo vitu wanaangalia kama utakuwa uwanjani na akili yako ipo nyumbani ni ngumu kutoa kilichokusudiwa ili kuosaidia timu ,kama mchezaji unatakiwa kuwa bora pia eneo hili jitahidi sana kujiweka mbali na vitu vitakavyochukua akili na fikra yako ili kulinda daraja lako


3.Physical fitness 

Maarifa na mbinu vina nafasi kubwa sana uwanjani lakini urahisi wa kuhamisha kilicho kwenye mawazo kuwa uhalisia uwanjani inakuhitaji kuwa na utimamu wa mwili , sehemu inayohitaji ukakamavu kakamaa , inapohitajiks kasi kimbia ! utimamu wa mwili ni silaha kubwa ya mchezaji.


4.Study the game 

Hii ni sehemu ya mbinu , zipo mbinu utapewa na mwalimu lakini zipo mbinu zitakuhitaji wewe mwenyewe kujiongeza. Kama mchezaji tenga muda wa kujiongezea mbinu na maarifa , njia za kujiongezea mbinu zinaweza kuwa kuangalia mechi tofauti tofauti, kuangalia wachezaji wakubwa wa nafasi yako wanatafsiri vipi matukio ,mwisho yafanyie kazi maarifa unayoyapata nje kuongeza kitu kwenye career yako ! 


Hivi ni vitu vinne muhimu ambavyo watu wa mpira wanapaswa kufahamu hasa wachezaji ili kujijenga na kuwa bora kila wakati.


DIGALA.

Post a Comment

0 Comments