Jezi namba 27 mgongoni. Uwanjani anakaa eneo la namba 8 Na Jukumu lake ni Box to Box Midfielder.
Ndiye mchezaji mwenye jukumu la kuipa Balance nzuri @yangasc kwenye nyakati mbili kubwa kiwanjani. Kujilinda na Kushambulia.
Mikimbio yake huipa @yangasc namba nzuri ya watu kwenye Boksi la mpinzani pindi timu inaposhambulia
‘Offensive’ ni mtu mzuri kwenye pasi, mikimbio mizuri ya kuwa kufika kwenye eneo sahihi kwa wakati sahihi .. Na kubwa zaidi ANAJUA KUFUNGA.
Movements za haraka za @mudathir_yahya27 kwenye boksi la mpinzani hutoa Faida kwa mchezaji mmoja kati ya wale watatu wa juu [Pacome, Maxi na Aziz Ki] kujikuta yuko huru na nafasi ya pasi huonekana..
Hapo inahitaji uwe na Taaluma kidogo ya Football kuona kisichoonekana.
Defensive. Wengi ukiwauliza kazi ya Muda pindi timu haina mpira watakwambia Pressing.
Yes, Wako sahihi Lakini .. Lakini Jicho zuri la Football litamuona @mudathir_yahya27 kwenye uwezo wake wa kuzuia njia za mpira.
Mpira unaweza kupotea kwenye eneo la juu, Lakini Movements zake za haraka kurudi kwenye njia za mpira huikoa sana @yangasc isidhurike na Counter Attack
Hili huwezi kuliona kwa jicho la kawaida .. Hata huwezi kulisikia wachambuzi wakilisema kwa sababu sio wengi wana Taalamu ya Football..
Siku Football ikianza kutazamwa na kupimwa ubora wa Taarifa za kiufundi zinazotokeq uwanjani.. Wachezaji aina ya @mudathir_yahya27 WANAWEZA KUSHINDA TUZO NYINGI KUBWA KWENYE MPIRA 👊
Kipaji Kikubwa sana hiki @mudathir_yahya27 🔰
0 Comments