Hot Posts

6/recent/ticker-posts

KAMA ZALI SUB YA BOKO IMEMBEBA KOCHA WA SIMBA


Simba ilifanya mabadiliko ya kwanza mwanzo wa kipindi cha pili akitoka Jean Baleke nafasi yake ikichukuliwa na nahodha, John Bocco na dakika kumi baadaye tangu aingie alipoteza nafasi ya wazi shuti lake lilitoka nje kidogo akipokea pasi ya kiungo Clatous Chama.
.
Baada ya kupoteza nafasi hiyo mashabiki wa Simba walirusha chupa za maji wakichukizwa na hatua hiyo ya kupoteza nafasi hiyo. Hata hivyo, Bocco aliziokota na kuzisogeza nje kidogo huku Chama akiwatuliza mashabiki hao lakini Bocco ndiye aliyeiokoa Simba dakika ya 68 baada ya krosi yake kusababisha beki wa Dynamos Kondwani Chiboni kujifunga wakati akijaribu kuokoa. 
.
Baada ya kuingia kwa bao hilo Bocco alilazimika kuwanyamazisha kwa kuwaonyeshea ishara ya kuwafunga midomo mashabiki waliojaza uwanjani ambao awali walionekana kutofurahia kuingizwa kwake kumpokea Jean Baleke.

 

Post a Comment

0 Comments