Hakuna timu Duniani isiyofungwa na kupoteza mechi, hakuna habadani labda ucheze Mwenyewe huku umejiwekea magoli na Uwanja wako hapo sawa
Tangu niujue mpira YANGA SC imeshapoteza michezo mingi tu na hiyo inanipa kujua maana nzima ya football, Kuna kushinda, Kushindwa na Kutoka sare au Suluhu
Leo Yanga SC mbele ya Ihefu FC imekutana na ile kanuni moja wapo ya kupoteza mchezo
Hata hivyo ukigusa kidogo kwenye suala la kiufundi hii itamsaidia sana kocha Miguel Gamond kwani itajua ni mchezaji gani aanze na yupi akae benchi
Na ikitokea umeanzia benchi haimanishi wewe ni mchezaji mbaya, hufai hapana ni katika chaguo la Mwalimu na mbinu zake ili apate matokeo kwani timu ikishinda mnakuwa mmeshinda wote!!
Ligi ndio kwanza mbichi yaani ndio imeanza hivyo kwaiyo tuendelee kuwa wavumilivu na kupongeza hizi timu zingine zinapozifunga timu zetu Kubwa
Ihefu FC imeshinda lazima wapongezwe wasitafutwe wachawi kwenye Klabu ya Yanga SC na wakifanya hivyo watakuwa wanakiuka miiko ya mpira na kuzitotosha sheria zake
HAKUNA TIMU ISIYOFUNGWA KOTE DUNIANI, HAKUNAAAAA
0 Comments