✍🏻Unawapa credit kubwa sana Palace jinsi walivyokuwa wabapambana kupata ambacho walikuwa wamekifuata pale Old Trafford
1: Zuia kwa idadi kubwa ya wachezaji bila mpira katika 5-4-1
2: Achana na kuwa press Man United , bali mpira ukipotea rudi nyuma na funga space katikati ya uwanja waache pembeni wapige krosi
3: Ukipata mali hakuna kubutua , unawatumia Mateta kukaa nao , Ayew kutembea nao pembeni na Eze kutembea nao nyuma ya kiungo cha United
4: Mwisho Sam Johnstone fanya kazi yako golini . Easy point tatu wanarudi nazo London ( Nyie bakini kushinda mechi ya Carabao Cup )
✍🏻Man United sijui unaanzia wapi ?
1: Chaos football . Hakuna utulivu , kila kitu kinafanywa haraka haraka .
2: Decision making : Sehemu ya kucheza mpira rahisi , wanaufanya mgumu . Pasi rahisi , inaongezewa ugumu
3: Casemiro , Amrabat zinachezwa rafu ambazo hazina ulazima kabisa kuwapa faida Palace pale ambapo nawataka kupumua .
NOTE
1: Kwani United wanacheza soka la namna gani ?? ETH anahitaji kujibu hili pia ( ni muda wa kutoka kwenye kichaka cha Glazers , inajulikana tatizo sugu lakini na yeye ana mzigo wake wa lawama .
2: Lile goli la Andersen utasema kafunga Zidane 🔥
3: Ila Rashford ? 🤔🤔🤔
4: Kafundishwa kwenye academy ya United , katikati ya wiki kapigwa chuma 3 leo kasema hampati kitu . Saves mbili nzuri ( Sam Johnstone )
5: Mechi 7 za EPL na tayari United kafungwa 4
FT: United 0-1 Palace
Wolves kwani naye kafanyaje huko ?? Nyie hii ligi hii daah 😀😀😀😀
0 Comments