Ipo mjadala mbalimbali kuhusu nani alicheza zaidi ya mwingine katika mchezo wa jana katika Stars na Algeria, inashangaza
Hivi tutaacha lini hizi mambo, pale imecheza Stars hakukua na Simba wala Yanga, hao wakina Kibu Denis na Ibrahim Baka, alivaa jezi ya Tanzania kulipambania Taifa sasa huo ubaguzi wetu unakuja vipi hapo
Akicheza vizuri Kibu akiwa Stars anapaswa kupongezwa na watu wote huku tukiisifu Stars iwe hivyo pia kwa Dickson Job na wengine tusilete lawama za kibaguzi
Kiukweli hii timu inatupwa sana inakuwa pendwa kama hivi imetokea limefanyika jambo mbali na hivyo hakuna mtu ana mpango nayo kabisa
Ngoja utaona hiyo mwakani kule Ivory coast kila mmoja atajifanya anahusika na kujipa majukumu na kuonekana TAIFA STARS ni ya kwake 😂😂
Nimalizie tu, tuipende Stars katika nyakati zote na tupunguze ubaguzi wa Usimba na Uyanga ndani ya Stars 🙏
0 Comments