Tunachojaribu ni kutiana unyonge tu ila siyo poa, kama wachezaji wetu wa hizi timu wametumia usafiri ule wa Anga, hizi mada ni za nini
Niko njiani naikaribia NDOLA kwa huo usafiri unaosemwa kwa masimango huku tukifurahia maisha na wana Simba SC Kutoka Tawi maarufu nchini la Kamati ya roho mbaya
Hao ambao wamechagua usafiri wa Coaster siyo kitu kibaya Kubwa wafike na wakaipe timu yao nguvu kama ambavyo hata sisi huku Zambia tumejipanga kuishangilia SIMBA SC pamoja na majukumu yangu ya kiuandishi
Sikutaka kuliandika hili ila tu tunajaribu kushushana katika level za haya mashindano, michuano mikubwa barani Afrika
SIMBA SC yeye yupo zake Zambia tupige goti tuiombee ishinde huku huku na game imalizikie hapa, vivyo hivyo kwa Yanga SC ambao wapo Rwanda, huo ndio Uzalendo wa kweli
Ndani ya hii Coastal tunaburudika kwa mziki mzuri, maongezi ya hapa na pale Kutoka Kwa mashabiki wa Mnyama yaani ni raha tu
Unataka kusema wamiliki wa hizo Coaster waache Biashara kwakua tunajua tu kuna mabasi makubwa, ni hoja mfu Kabisa tukatae propaganda hizo
0 Comments