Hot Posts

6/recent/ticker-posts

FEITOTO ANATESWA KISAIKOLOJIA NA YANGA


🗣️ Katika mchezo wa jana wa Azam fc dhidi ya T prison klabu ta Azam fc ikipata ushindi wa mabao matatu kwa moja, Kiungo Feisal alipata nafasi ya kucheza na kutolewa kikosi kwenye dakika za kipindi cha pili, katika ushindi huo feitoto hakupata nafasi ya kupachika bao kwenye mchezo ingawa alipata nafasi zaidi ya tatu ambazo hazikuweza kulenga lango.

🗣️Fei toto ukimwangalia mpaka sasa ni kama anapambana na maneno ya wadau wa soka hapa Tanzania na Mashabiki wa Yanga ambao wanamuangalia atafanya nini ndani ya klabu ya Azam fc, Katika mchezo wa jana Fei analazimisha kufunga goli hata kama hakuna nafasi nzuri kwa upande wake kupachika bao, Pia anataka kufanya vitu vingi ndani ya uwanja ili aonekana yuko bora katika kikosi chake hii ni mbaya sana anatakiwa aachane na maneno ya mitandaooni na ajaribu kupambania klabu na sio mambo binafsi.

🗣️Kwasasa Fei anatakiwa apotezee maneno ya Mashabiki wa Yanga na maneno ya wadau yeye angalie maisha yake yake mapya pia aachane na habari za mitandaoni.



 

Post a Comment

0 Comments