Kuna wakati vyombo vya habari na Wananchi wengi Ulaya walikuwa wanachukizwa sana na tabia za Jose Mourinho na majigambo yake, walikuwa wanahisi ana dharau sana, ana kauli chafu sana na wengi wakabeba tafsiri kuwa sio Muungwana, siku moja alikuwa kwenye kikao cha Waandishi wa Habari akajibu tuhuma hizo
“Kuna watu wananiita kiburi na mjivuni, lakini wanasahau kuwa mimi ni Bingwa wa Ulaya, nadhani mimi ni The Special One” akazima kipaza sauti na kuondoka zake Jose Mourinho, ndio bingwa wa Ulaya aliyebeba UEFA akiwa na FC Porto, wala hakujali kitu kwakuwa alikuwa anafahamu kuwa anajua anachokifanya.
Namtazama sana Colorado King Hassan Mwakinyo, kuna wakati watu wanachukizwa na majigambo yake, ujivuni wake na maneno ya karaha lakini sote tunakubaliana eidha kwa siri ama hadharani, eidha bafuni ama chooni ukiwa mwenyewe, unakiri kuwa Mwakinyo ni The Special One wa zama hizi, namba zinambeba sana.
Huenda Mwakinyo hana bahati kwakuwa amezaliwa Tanzania ambapo kujua kitu kwetu tunaona dhambi, yani mtu akiitwa MJUAJI wanahisi ni kosa yani usijue kitu, ila Tanzania ina bahati sana kuwa na CHAMPEZ kwakuwa ni watu wachache wa aina yake na hawazaliwi kila vizazi na kila nyakati, its okay to be arrogant.
VISIT MOROGORO🇹🇿
0 Comments