✍🏻Kama kuna kitu Katwila atakuwa amefurahi sana ukiacha matokeo chanya dhidi ya Yanga , ni upambanaji wa wachezaji wake , kucheza bila hofu , na kuwa wafanisi mbele ya goli pale walipohitajika ( ongeza na kuzuia vizuri kuifunga mechi kabisa )
✍🏻Vitu vya msingi ambavyo ukicheza na timu ambayo unajua ni nzuri
1: Shinda mipambano yako , iwe hewani au chini
2: Hakikisha mpinzani wako anaipata mipira ya pili michache sana iwezekanavyo tena mbali na lango lako
3. Upeku kucheza faulo nyingi karibu na lango lako
4: Hakikisha una namba nzuri ya kushambulia pale ambapo unapata mpira
5: Nafasi za kufunga mara nyingi huwa zinakuwa chache ukicheza na timu nzuri , basi zile zinazopatikana kuwa mfanisi
6: Golikipa wako awe na mechi nzuri sana sio shot stopping tu bali sehemu muhimu nyingine ni kucheza sana krosi
Haya ndio mambo ambayo Ihefu FC wameyafanya kwa kiwango kizuri ndio maana wanabaki Mbeya na pointi zao zote tatu Vs Yanga SC
✍🏻Yanga SC sidhani kama watatoka uwanjani na kurejea DSM wakiwa wanasema ile mechi hatukustahili kupoteza
1: Hawakutengeneza nafasi nzuri za kufunga
2: Uharaka wa kufanya maamuzi
3: Hasa kipindi cha kwanza , idadi ya wachezaji waliokuwa wanaenda kushambulia ni wachache sana
4: Kipindi cha pili walicheza vile ambavyo Ihefu FC walikuwa wanataka .... mipira mirefu na kuubana uwanja wote wamekusanyika eneo moja kitu ambacho ni rahisi kuzuia ( maana yake wachezaji wa Ihefu hawakuhitajika kuzuia eneo kubwa la uwanja )
✍🏻Nafikiri kutoka timu zote mbili hakukuwa na passing game sana ,ni mechi ambayo ilihitaji mikakati tofauti kushinda
NOTE
1: Ndio Tigere kapiga freekick vizuri lakini Diarra alipaswa kufanya vizuri zaidi ya pale . Goalkeeping mistake
2: Ukisikia kujituma ili kupata matokeo chanya basi ndio Ihefu walivyofanya
3: Ilanfya kwenye goli lake 🔥🔥 kwanza mpira mrefu kauwa chini, kaweka mali pembeni then hajasimama kaendelea na safari yake : Pasi ya Mahundi , na dummy ya Shaban , Finishing ya Ilanfya super goal
4: Kissu na Nyosso 🔥
5: FIKIRINI umbile lake lisikudanganye 🔥Good performance
FT: Ihefu FC 2-1 Yanga SC
0 Comments