Hot Posts

6/recent/ticker-posts

NEWCASTLE NI TIMU KONGWE UINGEREZA WANAOGAWA DOZI KWENYE UEFA MSIMU HUU


Newcastle ni moja kati ya timu kongwe na yenye mafanikio England, msimu huu Magpies chini ya Eddie Howe wanauwasha moto kwenye UEFA wakiongoza kundi lao mbele ya PSG, Dortmund na AC Milan ambapo wawili wa mwisho wana taji la UEFA tayari.

PSG amekubali chuma 4-1 ambapo ni kipigo kikubwa zaidi kwao ndani ya michuano hiyo tangu waarabu wa Qatar waichukue timu QSI Group, huku ukiwa ni usiku mzuri zaidi ndani ya Mtakatifu James.

Mashabiki maarufu wa Newcastle hapa nchini Tanzania ni Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwamuzi wa pembeni Frank Komba, leo wanakula kuku tu Magpies @jakayakikwete @kombafrank

 

Post a Comment

0 Comments