Hot Posts

6/recent/ticker-posts

SIMBA WAMERUDI KWENYE HEADLINES TENA? WAWEKA MIPANGO YA KUIKABILI POWER DYNAMO


 

"Mchezo dhidi ya Power Dynamos utachezwa siku ya Jumapili Oktoba mosi saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex. Tumeamua kucheza saa 10 sababu michezo mingi hapa karibuni tumecheza muda huo hivyo hatukutaka kubadili muda lakini pia Jumatatu itakuwa siku ya kazi hivyo tunataka watu wawahi kurudi nyumbani."


"Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ndio utafatiliwa zaidi Afrika kwa wikiendi hii kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza. Ukubwa wa Simba SC ndio unafanya mchezo huo uwe mkubwa zaidi."


"Kikosi leo kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Azam Complex pale Chamazi kwa ajili ya kuzoea uwanja. Tangu tumeanza msimu huu hatujawahi kutumia ule uwanja. Wapo wachezaji wetu wengi wanaujua uwanja ule na wpao wengine hawaujui."


"Wachezaji watatu watakosekana kwenye huo mchezo. Wachezaji hao ni Aishi Manula, Henock Inonga na Aubin Kramo."- Ahmed Ally. #WenyeNchi #NguvuMoja


"Viingilio tumeweka rafiki lakini pia tukubaliane uwanja wa Azam Complex ni uwanja mdogo. Kwenye mchezo kama huu msimu uliopita tuliingiza watu 47,000 lakini sasa tutakuwa na mashabiki 7,000. Mashabiki wanaotaka kuwepo uwanjani wanunue tiketi haraka."


"Tiketi za Mzunguko ni Tsh. 10,000, VIP B ni Tsh. 30,000 na Platinum ni Tsh. 150,000 ambayo utapata zawadi, usafiri, chakula ukiwa uwanjani. Watu wanasema Chamazi ni mbali lakini watu wa Platinum Chamazi sio mbali maana wana basi na escort."- Ahmed Ally. #WenyeNchi #NguvuMoja

"Power Dynamos wanatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi majira ya saa 12 jioni na shirika la ndege la ATCL. Waamuzi wanatarajia kufika Tanzania tarehe 30 Septemba."


"Huu mchezo CAF wanauangalia, wanaangalia timu ya CAF Football League. Itakuwa ni aibu eti timu ya CAF Football League alafu isiwepo hatua ya makundi."- Ahmed Ally. #WenyeNchi #NguvuMoja

Post a Comment

0 Comments