Hot Posts

6/recent/ticker-posts

HAYAWI! HAYAWI! HATIMAYE FAINALI NDONDO CUP NI LEO


 Msimu wa 10 wa Ndondo Cup unahitimishwa leo kwa mchezo wa Fainali kati ya KIBANGU RANGERS dhidi ya MADENGE FC, bingwa mpya wa Ndondo Cup 2023 atavikwa ufalme👑 na mitaa itapiga salute kwa heshima.


Wenyeji wa mchezo Kibangu Rangers wameingia Fainali ya Ndondo Cup kwa mara ya kwanza. Historia ipo upande wao kwakuwa katika misimu 9 iliyopita hakuna bingwa aliyewahi kutetea ubingwa!


Madenge FC wanashiriki Ndondo Cup kwa mara pili, msimu uliopita ulikuwa wa kwanza kwao kwenye mashindano haya. Walianzia hatua ya awali hadi Fainali na kuchukua kombe. 


Msimu huu wameingia Fainali kwa mara nyingine na kuifikia rekodi ya Kauzu FC kucheza Fainali mbili za Ndondo Cup, wadau wengi wanataka kuona kama Madenge itaweza kuweka rekodi mpya ya bingwa pekee aliyetetea kombe.


Nahodha wa Kibangu Rangers Mushda Khamis amecheza Ndondo Cup tangu msimu wa kwanza! Huu ni msimu wake wa 10 anacheza Ndondo Cup akiwa na timu tofautitofauti na hii ni Fainali yake ya kwanza! Je, atafanikiwa kunyanyua ndoo leo?


Star wa Madenge FC Mashaka Pogba pia huu ni msimu wake wa 10 anacheza Ndondo Cup! Leo anacheza Fainali kwa mara ya pili mfululizo akiwa na Madenge FC, msimu uliopita alinyanyua ndoo leo anatafuta rekodi ya kuvaa medali ya pili mfululizo ya ubingwa wa Ndondo Cup.

Post a Comment

0 Comments